Jumatatu 26 Januari 2026 - 02:00
Marekani na utawala wa Kizayuni hawana uwezo wa kuidhuru Iran

Hawza/ Ayatullah Jawadi Amoli, huku akiongoza dua kwa ajili ya kulindwa mfumo wa Kiislamu, alisisitiza kuwa: Marekani na utawala wa Kizayuni hawana uwezo wa kuidhuru njia hii, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mfumo huu utabakia salama na kamili mikononi mwa mwenye haki yake halisi, yaani Hadhrat Waliyyul-Asr (a.j.).

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amoli mwanzoni mwa kikao cha somo lake la fiqhi la tarehe 25 January, kwa kuashiria maadhimisho ya kuzaliwa kwa baraka ya Imam Sajjad (a.s.), alifafanua nafasi ya msingi ya dua na "Risalatul-Huquq" ya Imam huyo mtukufu.

Akasema: Imam Sajjad (a.s.) aliwasilisha mpango kamili kwa maisha binafsi na ya kijamii ya mwanadamu; kwa mtazamo wake, dua si kuomba haja tu, bali ni mwongozo kamili unaomwelekeza mwanadamu asipotoke njia wala kuzuia njia ya wengine, na ajihisi kuwa na wajibu mbele ya nafsi yake, familia yake na jamii.

Ayatullah Jawadi Amoli aliongeza kiwa: Dua za kila wiki za Imam Sajjad (a.s.), ambazo zimetajwa mahsusi kwa kila siku ya wiki, ni mpango uliopangiliwa vyema na wa malezi unaoratibu maisha ya Kiislamu ya muumini.

Aidha, alieleza kuwa: Mbali na mpango huu wa kila wiki, kuna sehemu nyingine ya dua za Imam Sajjad (a.s.) zinazohusiana na hali na matukio maalumu ya maisha; kwa maana kwamba kwa kila hali na kila tukio, kuna dua maalumu iliyowekwa ambayo huchukua nafasi ya mwongozo wa vitendo.

Alisisitiza: Sehemu hizi mbili — yaani mpango wa kila wiki na dua za matukio mbalimbali — ni sura mbili za kielimu zilizo tofauti lakini zinazokamilishana.

Ayatullah Jawadi Amoli, akirejelea "Risalatul-Huquq" ya Imam Sajjad (a.s.), alisema: Sura muhimu zaidi ni suala la haki; yaani jinsi ya kuwa mwanasiasa sahihi, jinsi ya kuwa mtaalamu wa jamii, namna ambavyo binadamu anapaswa kuwa na uhusiano na mfumo, jamii, watu na familia, na kila mmoja ana haki zipi.

Alibainisha: "Risalatul-Huquq" si maandiko ya kimaadili pekee, bali ni risala ya kielimu na kivitendo kwa ajili ya kupanga na kusawazisha mahusiano ya kisiasa, kijamii na kifamilia.

Ayatullah Jawadi Amoli alikumbusha kuwa: Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mhukumu wa mahitaji, Mfungua milango na Mponyaji wa maradhi, lakini kila dua ina nafasi na mahali pake mahsusi, na Imam Sajjad (a.s.) ametufundisha mpangilio huu makini.

Ayatullah huyu mkubwa alitaja mkusanyiko huu wa pande tatu wa mafundisho ya Imam Sajjad (a.s.) — dua za kila wiki, dua za matukio maalumu na "Risalatul-Huquq" — kuwa ni hazina yenye manufaa makubwa kwa jamii ya kisasa iliyoendelea, na akasema: Maarifa haya yanapaswa kutafsiriwa, kufafanuliwa na kufanywa ya vitendo na wenye dhamana, kwa ngazi mbalimbali za jamii; kwa vijana, balehe, watu wazima na familia, kila kundi kwa lugha inayolingana nalo, ili uongozi wa Imam huyo uweze kuishi na kutekelezwa katika vitendo.

Akiwekea mkazo juu ya nafasi ya tawakkul (kumtegemea Mwenyezi Mungu) na kumuomba Yeye moja kwa moja, alisema: Mara nyingi tunaomba mambo mengi kutoka kwa watu mbalimbali lakini hatufikii matokeo, ilhali kama tungeanza kwa kumuomba Mwenyezi Mungu, Yeye angeongoza na kuonesha njia. Wakati mwingine tatizo halitatuliwi kwa njia ya ghaibu, bali kwa uongofu wa Mwenyezi Mungu kupitia ushauri wa mtu sahihi ambaye Mwenyezi Mungu humweka akilini mwa mtu.

Mwisho wa hotuba yake, huku akisoma dua ya kulindwa kwa mfumo wa Kiislamu, Ayatullah Jawadi Amoli alisema: Marekani na utawala wa Kizayuni hawana uwezo wa kuidhuru njia hii, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mfumo huu utafika salama na kamili mikononi mwa mwenye haki yake halisi, Hadhrat Waliyyul-Asr (a.j.).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha